
Ndugu wawekezaji mnakumbushwa kuwa Taarifa inatolewa kwa umma kwamba kuanzia tarehe 12 Disemba 2022,
Yetu Microfinance Bank PLC imewekwa chini ya usimamizi wa Benki Kuu
ya Tanzania, msimamizi mkuu wa Sekta ya Benki, kwa kipindi kisichozidi
siku tisini (90), baada ya kipindi hicho, Benki Kuu itatoa uamuzi stahiki.
Wawekezaji wanashauriwa kuzingatia taarifa hii wanapofanya uamuzi wa
kuwekeza kwenye dhamana za YETU Microfinance Bank PLC.
Imetolewa na:
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu
SOKO LA HISA DAR ES SALAAM